Wahisani na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu wahimizwa kujitokeza na kumsaidia na ufadhili wa karo Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Ganda kule Malindi Cheryl Awour Opondo.
Awour alipata alama 420 katika mtihani wa KCPE ambao matokeo yake yalitangazwa na Waziri wa Elimu nchini Profesa George Magoha.
Kulingana na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Nicholas Mwangala, Awour ni mwanafunzi mwerevu na anahitaji msaada huo kwani anapitia maisha magumu baada ya kumpoteza mamake mzazi na babake anakabiliwa na changamoto za kiafya.
Naye shangaziy wa Awour, Jackline Omondi amewasihi wahisani kujitokeza na kumsaidia Awour kwa karo ya shule ili atimize ndoto yake ya masomo kwani kama familia wanapitia changamoto mbalimbali.
Hata hivyo Mwanafunzi huyo amewaomba wasihani kumsaidia kimasomo ili atimize ndoto yake ya kuwa daktari na kuisaidia familia yake.