Story by Hussein Mdune-
Wizara ya Elimu nchini imetangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE mwaka wa 2021 ambapo zaidi ya wanafunzi milioni 1.2 walifanya mtihani huo.
Akizungumza wakati wa halfa ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa KCPE katika makao makuu ya baraza la mitihani nchini KNEC jijini Nairobi, Waziri wa Elimu nchini Prof George Mahoha amesema wanafaunzi bora zaidi ni Magata Bruce Mackenzi kutoka shule ya msingi ya Gilgil hills Academy aliyepata alama 428.
Mwanafunzi wapili ni Momanyi Ashley Kerubo aliyepata alama 427, nafasi ya tatu ikishiliwa na Wanafunzi sita ambapo wote walipata alama 426 ambao ni Charity Buyanzi, Mbugua Sharon Wairimu, Muteti Shantell Linda, Stanley Otieno Omondi, Wekesa Naomi na Kimani Ethan Karuga .
Hata hivyo Waziri Magoha amewaonya walimu wakuu dhidi ya kuwanyima wanafunzi matokeo yao kutokana na madeni shuleni, akisema ni lazima wanafunzi wapewe matokeo yao licha ya changamoto hizo.
Wakati uo huo ameweka wazi kwamba mfumo upya wa elimu wa CBC umepiga hatua kwani walimu walipewa mafunzo ya ziada kufanikisha mfumo huo na tayari madarasa zaidi ya elfu 10 yamejengwa.
Kwa upande wake Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya kuajiri walimu nchini TSC Nancy Macheria amesema tume hiyo itawachukulia hatua za kisheria baadhi ya walimu waliopatikana na hatia ya kushiriki udanganyifu wa mtihani wa KCPE.