Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Aiport mjini Malindi kaunti ya Kilifi ana kila sababu ya kutabasamu baada ya kuandikisha matokeo bora zaidi kwa kupata alama 427 na kuwa mwanafunzi bora kutoka kaunti ndogo ya Malindi kwenye matokeo hayo ya KCPE.
Akiongea na wanahabari katika eneo la Airport baada ya walimu, wazazi kusherehekea ushindi wake Jonathan Maneno anasema kuwa licha ya changamoto ambazo amepitia wakati wa masomo alijizatiti na kuibuka na alama hizo.
Jonathan hata hivyo amesema kuwa ananuia kuwa daktari pindi atakapomaliza masomo yake katika shule ya upili ya Starehe ambayo ndio aliichagua.
Kwa upande wake mama wa mwanafunzi huyo Cecilia Mumba anaitaka serikali kufanya kila juhudi ya kumsadia karo ya shule za upili ikizingatiwa kuwa hana uwezo wa kifedha.