Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne katika eneo la Madogo gatuzi dogo la Bura kaunti ya Tana river amejifungua, siku ya pili ya mtihani wa kidato cha nne KCSE.
Akizungumza katika eneo hilo baada ya kuongoza zoezi la ufunguzi wa mtihani huo, Kamishna wa kaunti ya Tana River Thomas Sankei amesema mwanafuzi huyo amepelekwa katika hospitali ya Garissa anakoendelea kufanya mtihani wake akiwa na mwanawe mchanga.
Sankei amesema mwanafunzi huyo ataendelea kufanya mtihani wake hadi atakapotoka hospitalini, japo kwa sasa hali yake ni njema kiafya pamoja na mwanawe mchanga.
Sankei amesema mtihani huo umekuwa ukiendelea vyema tangu ulipoanza rasmi akisema maafisa wa usalama wanashirikiana kwa karibu mno na wasimamizi wa mtihani huo sawa na walimu na wanafunzi ili kuhakikisha hakuna kikwazo chochote kinachotatiza mtihani huo.