Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire amesema Kuna haja ya bunge la kitaifa nchini kubuni sheria maalum ya kukabiliana na visa vya mauaji ya wazee kwa tuhma za uchawi, Kilifi.
Mwambire amesema kuwa visa vya mauji ya wazee vinashuhudiwa katika kaunti hiyo kutokana na hatua ya jamii kuwa na dhana potofu. Amesema kupitia kwa sheria hiyo usalama wa wazee utaimarika.
Mbunge huyo aidha amesema licha ya kaunti ya Kilifi kuongoza kwa visa vya mauaji ya wazee kuna baadhi ya kaunti humu nchini ambazo visa hivyo vimeanza kichipuka,akiitaka serikali kuchukulia kwa uzito suala hilo.
Haya yanajiri huku visa vya mauaji ya wazee kwa tuhma za uchawi vikizidi kuongezeka hapa Pwani.
Taarifa na Hussein Mdune.