Afisa mkuu wa elimu eneo la Magarini kaunti ya Kilifi John Githinji amethibitisha kutimuliwa kazini kwa mwalimu mmoja wa shule ya msingi ya Kundeni eneo la Garashi kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi wawili shuleni humo.
Githinji amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya ripoti ya uchunguzi kubaini kuwa mwalimu huyo alihusika katika visa hivyo vya ubakaji.
Githinji amefichua kuwa mwalimu huyo aliwapeleka wanafunzi hao kichakani kabla ya kuwalazimisha kufanya nao tendo hilo na huenda amehusika katika visa zaidi ambavyo havikuripotiwa.
Taarifa na Esther Mwagandi.