Mkufunzi wa bandari Bernard Mwalala ametuzwa kama mkufunzi bora wa mwezi Agosti kwenye tuzo za kila mwezi za shirikisho la wanahabari wa michezo nchini SJAK kwa ushirikiano na kampuni ya bima ya Fidelity .
Akizungumza na wanahabari baada ya kupokea tuzo hiyo na hundi ya jumla ya Ksh75,000, Mwalala amesema kuwa tuzo hiyo imetokana na matokeo bora waliyoyapata baada ya kushinda mechi nne mfululizo za mwisho wa msimu uliopita.
Mwalala aidha amesema kuwa tuzo hiyo imempa motisha wa kukaribisha msimu mpya wa ligi kuu nchini KPL unatarajiwa kung’oananga Disemba 8.
Amesema kuwa wamefanya matayarisho ya kutosha na yuko tayari kwa msimu mpya unaokuja , Bandari itafungua msimu mpya ugani Mbaraki dhidi ya mabingwa watetezi Gor Mahia.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.