Mwakilishi wa wadi ya Sabaki kaunti ya Kilifi, Edward Dele, ametiwa nguvuni na maafisa wa polisi kwa kuhusika katika zoezi la kugawia wakaazi wa eneo hilo vipande vya ardhi katika shamba lenye utata la ADC.
Inaarifiwa kwamba mwakilishi huyo wa wadi ametiwa nguvuni pamoja na zaidi ya wakaazi 40 waliohusika katika ugavi wa shamba hilo hapo jana.
Imewalazimu maafisa wa polisi kutumia vitoa machozi kuwatawanya wakaazi waliokuwa wameandamana katika kituo cha polisi mjini Malindi kushinikiza kuachiliwa kwa kiongozi huyo.
Akizungumzia suala hilo Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi, Jimmy Kahindi amesema kuwa atatoa taarifa kamili kuhusiana na kukamatwa kwa mwakilishi huyo.
Taarifa na Radio Kaya.