Mwakilishi wa wadi ya Macknon road kaunti ya Kwale Joseph Tsuma Danda amehimiza ushirikiano wa serikali na wafadhili mbali mbali kufanikisha masuala ya elimu nchini ili kuboresha matokeo.
Danda amehoji kuwa wanafunzi wengi wa mashinani wanakumbwa na changamoto ya ukosefu wa karo hali inayopelekea wengi wao kusalia nyumbani.
Mwakilishi huyo wa wadi amesisitiza kwamba ufadhili unahitajika akisema kwamba pesa zinazotolewa kwa basari hazitoshi kukidhi mahitaji ya wanafunzi wote.
Kiongozi huyo amesisitiza kwamba wanafunzi wengi wakifadhiliwa visa vya ndoa za mapema katika kaunti ya Kwale vitapungua kwa kiwango kikubwa.
Taarifa na Hussein Mdune.