Ni sharti sheria inayosimamia hazina za akina Mama na Vijana humu nchini ipigwe msasa ili kuhakikisha hazina hizo zinawanufaisha walengwa.
Mwakilishi wa Kike kaunti ya Mombasa Asha Hussein amesema sheria zilizopo kwa sasa zinawafungia nje baadhi ya akina mama na vijana walio na maono ya kijiendeleza kiuchumi.
Akizungumza mjini Mombasa Asha amesema iwapo sheria hizo zitapigwa msasa na vikwazo mbalimbali kuondolewa, itakuwa rahisi kwa akina Mama na vijana kupata fedha za kuwekeza katika miradi ya kibiashara.
Kulingana na Kiongozi huyo ajira kwa Vijana imekuwa nadra na iwapo sheria hizo zitapigwa msasa na vijana kuhamasishwa jinsi ya kupata na kutumia fedha hizo basi changamoto zinazowakumba kiuchumi zitadhibitiwa.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.