Mwanahabari wa michezo James Oduor maarufu kama Cobra ni miongoni mwa watu 14 waliofariki katika shambulizi lakigaidi katika hoteli ya Dusit jijini Nairobi.
Oduor ni mwanzilishi wa kituo cha runinga kijulikanacho kama Wadau Tv kinachoangazia maswala ya michezo humu nchini.
Mwanaspoti huyu alikuwa nguzo muhimu katika tuzo kwa wanaspoti ambazo zimekuwa zikiendelea humu nchini kwa muda sasa.
Mungu amlaze pema alipochagua.