Story by Correspondents –
Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime ameitaka serikali ya kaunti ya Taita taveta kuwekeza miradi mikubwa ya maji ya safi ya kutumia kutoka kwa chemi chemi za maji za Njoro na Ziwa Chala katika eneo bunge la Taveta.
Mwadime amesema ni jambo la kushangaza kuona idadi kubwa ya wakaazi wa kaunti hiyo wakiendelea kutaabika katika kutafuta bidhaa hiyo muhimu licha ya kuwepo na suluhu la tatizo hilo.
Akizungumza katika eneo bunge lake, Mwadime ameitaka serikali ya kaunti ya Taita taveta kutenga mgao wa kutosha katika bajeti yake ya mwaka wa kifedha ili kufanikisha mIradi hiyo na kulitatua tatizo la uhaba wa maji.
Akigusia swala la uchumi wa nchini, Mwadime amesema wakaazi wengi kwa sasa wanapitia hali ngumu ya maisha kutokana na kudorora kwa uchumi wa nchi, akisisitiza haja ya mikakati ya kudumu kuidhinishwa.