Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime amewashinikiza waalimu katika kaunti ya Taita Taveta kuwasilisha changamoto wanazopitia kwa viongozi wao ili zikabiliwe.
Akihutubia waalimu mjini Voi Mwadime amesema kuwa waalimu hasa walioko katika shule za mashinani wanapitia changamoto lakini viongozi wao hawafahamu wa madhila wanayoyapitia.
Mwadime vile vile amemsihi katibu mkuu wa chama cha waalimu nchini KNUT Wilson Sossion ambae pia ni mbunge mteule kutumia fursa hiyo kuwasilisha lalama za waalimu kwa viongozi wakuu ilizikabiliwe.
Akigusia suala la uhaba wa waalimu Mwadime ameitaka tume ya kuajiri waalimu nchini TSC kuajiri waalimu zaidi katika kaunti hio ilikukabili changamoto iliopo kwa sasa.
Taarifa na Fatma Rashid.