Story by Bakari Ali-
Wizara ya Kilimo nchini imezindua mradi wa dola milioni 250 wa kuimarisha sekta ya Kilimo humu nchini, chini ya ufadhili wa benki ya dunia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika kaunti ya Mombasa, Waziri wa Madini, uchumi samawati na maswala ya ubaharia Salim Mvurya, amesema mradi huo utasaidia pakubwa taifa kujiimarisha kiuchumi.
Mvurya amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali kuu na zile za kaunti ili kuimarisha sekta ya Kilimo na ile ya uchumi samawati humu nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa sekta ya Kilimo katika baraza la magavana nchini, aliye pia Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka amesisitiza ushirikiano huo ili kuimarisha sekta ya Kilimo humu nchini.