Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya, amewahimiza vijana wa kaunti hiyo kujitenga na ushawishi unaoweza kuwaingiza kwenye utovu wa nidhamu.
Mvurya amesema ukosefu wa ajira umewaweka vijana wengi kwenye hatari ya kushawishika kwa urahisi na kufanya uhalifu.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa vifaa vya kufanyia biashara kwa makundi 11 ya vijana katika afisi za Shirika la Msalaba Mwekundu kule Mvindeni, Mvurya amewahimiza vijana kujishuhulisha zaidi na mambo ya kuwajenga kimaisha.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Abbass Gullet, amesema rais Uhuru Kenyatta aliidhinisha mradi huo miaka miwili iliyopita baada ya kufanya mkao na vijana kutoka kaunti 6 za ukanda wa Pwani.
Taarifa na Michael Otieno.