Story by Gabriel Mwaganjoni-
Waziri wa madini na uchumi wa baharini Salim Mvurya amesema serikali imeweka mipango inayolenga kufufua sekta ya uvuvi ili kuwafaidi wakaazi wengi pamoja na kuinua kipato cha taifa.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Mvurya amesema serikali inalenga kuimarisha shughuli za uvuvi pamoja na kuboresha mazingira ya uvuvi baharini.
Murya ameweka kwamba mikakati zaidi ya kuboresha sekta ya uvuvi inaendelezwa ili kuhakikisha wavuvi wa humu nchini wanakuwa na nafasi ya kuvua samaki katika maeneo ya katikati mwa bahari hindi ya Kenya.
Wakati uo huo amedokeza kwamba tayari serikali imetenga maeneo yatakayoekezwa bandari ndogo ndogo za kuhifadhia vifaa vya uvuvi pamoja na maeneo ya kuhifadhi samaki katika maeneo tofauti pambizoni mwa bahari hindi ya ukanda wa Pwani.