Taarifa na Mwanaamina Faki.
Huku kamati ya bunge la seneti kuhusu bajeti ikiendelea kukagua miradi iliodhinishwa katika kaunti ya Kwale,viongozi kaunti hio wamepata wakati mgumu kujibu maswali mbele ya kamati hio kuhusu kutotumika kwa soko na uwanja wa mpira eneo la Msambweni licha ya miradi hio kukamilika miaka mitano iliopita.
Akiongea mbele ya kamati hio kwa niaba ya Gavana Salim Mvurya ,waziri wa michezo Kaunti ya Kwale Ramadhan Bungale amejitetea akisema kuwa soko hilo limekosa kutumika kutokana na ukosefu wa umeme eneo hilo.
Kwa upande wake Mwakilishi wadi ya Ramisi ambae pia ni kiongozi wa walio wengi katika bunge la Kaunti ya Kwale Raia Mkungu ameilaumu serikali ya kaunti hiyo kwa kuidhinisha miradi kwenye ardhi zilizo na utata hali inayochelesha kutumika kwa miradi hio.
Kamati ya bunge la seneti kuhusu bajeti hii leo imezuru maeneo ya mashinani kaunti ya Kwale kukagua miradi iliotekelezwa na serikali ya kaunti ,ilikuhakikisha miradi hio inafikia viwango vya fedha iliotengewa.