Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya ameipongeza Mahakama ya Upeo kwa kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi mkuu uliopita.
Akihutubia Wanahabari baada ya uamuzi wa Mahakama hiyo akiwa katika kijiji cha Saba saba, eneo la Matuga kaunti ya Kwale, Murya amewaomba wakwale kushirikiana naye ili kuendeleza kaunti ya Kwale katika maswala mbalimbali ya maendeleo.
Amesema ushirikiano, umoja na mshikamano ndio ufasini wa kaunti ya Kwale katika kufanikisha ujenzi wa kaunti hiyo.
Kwa upande wake Mshenga Vuyaa Ruga mmoja wa Wakurungezi katika bodi ya Halmashauri ya Maendeleo Pwani, akimtaka aliyekuwa mgombea wa kiti cha Ugavana kaunti ya Kwale kupitia chama cha Wiper Balozi Chirau Ali Mwakwere kushirikiana na Mvurya kwa ajili ya maendeleo ya wakaazi wa Kwale.
Taarifa na Mariam Gao.