Story by Our Correspondents-
Muungano wa One Kenya Alliance yaani OKA umeweka wazi kwamba kuna mazungumzo mpya yanayoendelea kati ya OKA na chama cha Jubilee na ODM ili kubuni Muungano mpya kwa jina Azimio One Kenya Alliance.
Vinara wa Muungano huo wa OKA wakiongozwa na Kalonzo Musyoka wamesema wanatarajia kukamilisha mazungumzo hayo kabla ya siku ya Jumatatu ili kuwasilisha jina la Muungano huo kwa msajili wa vyema vya kisiasa nchini.
Kalonzo amesema mazungumzo hayo yatazaa matunda na kuchangia kuendelea kwa taifa hili na kushuhudia uongozi bora.
Wakati uo huo amewasi wakenya kuzidi kuliombea taifa hili sawa na kudumisha amani huku akivirai vyama vyengine vya kisiasa kujiunga na mpango huo.