Story by Our Correspondents-
Jopo la watu 7 lililoteuliwa na viongozi wakuu wa Muungano wa Azimio la umoja One Kenya kuwapiga msasa viongozi wanaotaka kuteuliwa kama mgombea mwenza wa Raila Odinga limeanza rasmi zoezi hilo.
Jopo hilo ambalo linajumuisha Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki Zacchaeus Okoth, Senator Enoch Wambua, Michael Orwa, Dkt. Noah Wekesa, Sheikh Mohamed Khalifa na Beatrice Askul Moe wanatarajiwa kuibuka na jina la mtu mmoja atakayekuwa mgombea mwenza wa Odinga.
Mkurugenzi wa uchaguzi katika chama cha ODM Junet Mohemmed amesema jopo hilo lina hadi tarehe 10 ya mwezi huu ambapo litatangaza rasmi mgombea mweza wa Odinga kwani jopo hilo lina watu wenye tajriba ya hali ya juu.
Wagombea wanaomezea mate nafasi hiyo ni pamoja na Kinara wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Martha Karua wa Narc Kenya, Gavana wa Kitui Charity Ngilu, Mbunge wa zamani wa Gatanga Peter Kenneth na Waziri wa Kilimo nchini Peter Munya.
Hata hivyo Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imewapa mda wa hadi tarehe 16 mwezi Mei mwaka huu wagombea wote wa urais kuhakikisha wametuma majina ya wagombea wenza kwa tume hiyo.m