Picha kwa hisani –
Inspekta mkuu wa polisi nchini Hillary Mutyambai amewaagiza maafisa wa usalama kuanza kuwahimiza wakenya kuzingatia kikamilifu masharti yaliotolewa na serikali kuhusu juhudi za kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.
Mutyambai amesema hatua hiyo inaanza na kutia mkazo masaa ya kafyu ambayo yanaanza saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri huku akiwaonya watakaokiuka masharti hayo kuwa watakabiliwa kikamilifu.
Mutyambai amesema watakaopatikana na hatua ya kutovaa barakoa katika maeneo ya umma, watatozwa faini ya shilingi elfu 20 bila ya kuruma, huku akisisitiza kuwa ni lazima kila mmoja achukue jukumu la kujikinga.
Wakati uo huo amewahimiza wakenya kuzingatia kikamilifu masharti ya kujikinga dhidi ya Corona kwa kuvaa barakoa katika maeneo ya umma, kuosha mikono kila mara sawia na kujitenga na mikusanyiko ya watu.