Picha Kwa Hisani –
Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavavi amemtaka Rais Uhuru Kenyatta Kuunda tume ya kisheria itayochunguza ile sakta ya wizi wa fedha za umma katika Taasisi ya kusambaza dawa nchini Kemsa.
Mudavadi amesema Rais Kenyatta ana uwezo, kisheria wa kuunda tume itakayowachunguza wale waliohusika na ufisadi katika wizara ya afya na taasisi hiyo ya Kemsa.
Mudavadi ametaja kuwa anaungana na wakenya kulaani hatua ya watu wachache kutaka kujinufaisha kupitia janga la Corona.
Mudavadi ameongeza kusema kuwa hatua hiyo itaondoaa propaganda zinazoenezwa kuhusu baadhi ya watu wanaotajwa kuhusika katika ubadhirifu wa fedha za umma.
Aidha kiongozi huyo amesisitiza iwapo hatua hazitachukuliwa dhidi ya wafisadi basi jambo hilo lichukuliwa kuwa mtindo wa kawaida.