Picha kwa Hisani –
Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi amewatahadharisha Wakenya dhidi ya siasa za udanganyifu na hadaa.
Mudavadi amesema siasa zinazoendelezwa nchini kwa sasa sio za ukweli na ni lazima wakenya wazinduke na kuwathamini viongozi wakweli na waliyo na nia njema kwa taifa hili.
Mudavadi amesema ni wazi wanasiasa wanaomiliki kampuni za kutoa fedha na bidhaa mbalimbali hawatawaongoza vyema wakenya bali watanuia kujilipa gharama zao pindi watakapoingia uongozini.
Kiongozi huyo wa ANC anayewania urais katika uchaguzi mkuu ujao amewataka Wakenya kushirikiana na viongozi waliyo na nia ya kuufufua uchumi wa nchi na wala sio viongozi wa kuwapa fedha chache.