Picha kwa Hisani –
Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi amewatahadharisha Wakenya dhidi ya siasa za uchochezi.
Mudavadi amesema tayari wakenya wamegawanywa kwa kuhadaiwa na wanasiasa akiwataka wakenya kuwa watulivu na kujiandaa kuubadilisha uongozi wa taifa mwaka wa 2022.
Wakati uo huo,Mudavadi amesema hatatikiswa katika azma yake ya kuunyakua urais wa taifa hili.
Wakati uo huo, Seneta wa Kaunti ya Kakamega Cleophas Malala amewakosoa wale wanaodai kwamba chama cha ANC kimesambaratika akisema chama hicho kiko imara na kinalenga kubadili siasa za nchi.