Story by Bakari Ali –
Serikali za Gatuzi zimehimizwa kushirikiana na serikali kuu ili kuimarisha sekta ya Kilimo humu nchini.
Akizungumza katika kongamano la wadau mbalimbali wa sekta ya Kilimo katika kaunti ya Mombasa, Waziri wa Kilimo nchini Peter Munya amesema ni sharti serikali hizo kushirikiana na kutatua changamoto zinazoikumba sekta hiyo.
Munya amesema changamoto zinazoikumba sekta hiyo ni pamoja na kupuuzwa kwa sekta hiyo humu nchini hali ambayo imechangia kuathirika kwa sekta hiyo kutokana na kuagizwa kwa bidhaa mbalimbali za Kilimo kutoka kwa mataifa ya kigeni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Kilimo katika serikali za kaunti James Nyoro ambaye pia ni Gavana wa Kiambu amesema serikali za kaunti zitakuwa zikitenga asilimia 10 ya bajeti ya kila mwaka ili kuimarisha sekta hiyo humu nchini.