Story by Our Correspondents-
Waziri wa Kilimo nchini Peter Munya amewashtumu viongozi wa Mrengo wa Kenya kwanza kwa kuendelea kuikosea serikali licha ya kuendeleza juhudi za kupambana na gharama ya maisha nchini.
Akizungumza katika mikutano ya kisiasa ya Odinga, Munya amesema ni makosa kwa viongozi hao hasa Naibu Rais William Ruto kuikosoa serikali ilhali ni kati ya viongozi wakuu serikaini ambao wanapaswa kushirikiana ili kulitatua tatizo hilo.
Munya anadai kushangazwa na viongozi ambao bado wako ndani ya serikali ilhali wanaendelea kuikosoa serikali badala ya kuibuka na suluhu la kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Wakati uo huo amewataka wakenya kuwa makini wanapofanya maamuzi ya kuwachagua viongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9, ili kuepuka kuwachagua viongozi wasio na maadili.