Story by Charo Banda:
Seneta wa kaunti ya Tana-river Danson Mungatana ameendeleza mpango wa kuelimisha wakaazi wa eneo bunge la Galole kuhusu umuhimu wa kuelewa utendakazi wa serikali za kaunti.
Mungatana katika hotuba yake amesema huenda Gavana wa Tanariver Dhadho Godhana akahitajika kufika mbele ya bunge la Seneti ili kueleza jinsi anavyotekeleza miradi yake katika kaunti hiyo.
Wakaazi wa kaunti hiyo hata hivyo wamelalamika kwamba serikali ya kaunti ya Tanariver imekua ikiidhinisha miradi ya maendeleo bila ya kuwashirikisha kupitia vikao vya kukusanya maoni ya umma.
Hata hivyo imebainika kwamba idadi kubwa ya wakaazi wa kaunti ya Tanariver hawajapewa mafunzo kuhusu jinsi ya kufanya uangalizi wa miradi ya maendeleo inayoidhinishwa katika kaunti hiyo.