Story by Ngombo Jeff-
Serikali ya kaunti ya Kilifi inalenga kuandaa kongamano na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo ili kujadili hatua mpya za kufufua kilimo cha korosho.
Gavana wa kaunti hiyo Gedion Mung’aro, amesema serikali ya kaunti hiyo tayari imepata mfadhili aliye na mbegu za kisasa za mkorosho zilizo na uwezo wa kukua kwa haraka.
Mung’aro aidha amedokeza kwamba viwanda viwili vya korosho viko katika harakati ya kukamilishwa kujengwa katika eneo la Vipingo na kile cha Kakanjuni ambacho kinajengwa kupitia ufadhili wa taifa la Czech na USAID.
Wakati uo huo ameweka wazi kwamba serikali ya kaunti hiyo itaanza kutoa mbegu za mkorosho kwa wakulima hivi karibuni ili kufanikisha mpango huo.