Picha Kwa Hisani
Mume wa marehemu mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Nigeria Osinachi Nwachukwu amekamatwa kufuatia kifo chake, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti.
Osinanchi, 42, alipoteza maisha siku ya Ijumaa akiwa hospitalini katika mji mkuu, Abuja.
Picha Kwa Hisani.
Taarifa za awali zilisema kuwa mwimbaji huyo maarufu alikuwa akiugua saratani ya koo, lakini familia yake inakanusha hilo, ikidai kuwa alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.
Lakini Msemaji wa polisi mjini humo amenukuliwa na tovuti za Daily Trust and Punch akithibitisha kukamatwa kwa Peter Nwachukwu baada ya malalamiko kutoka kwa kaka yake mwimbaji huyo.
Haijabainika iwapo Bw. Nwachukwu ametoa maoni yake kuhusu kukamatwa kwake.
Picha Kwa Hisani.
Osinachi alipata umaarufu 2017 kwa wimbo wa injili Ekwueme aliouimba na Prospa Ochimana.
Pia alikuwa mwimbaji mkuu Dunamis International Gospel Centre.