Picha / kwa hisani.
Polisi katika eneo la kisauni wanamtafuta mwanamume mmoja aliyemuuma na kumkata mdomo mkewe.
Kulingana na taarifa kutoka kwa kituo cha polisi cha Bamburi ni kuwa mwanamume huyo anayefahamika kwa jina la David alikuwa na ugomvi na mkewe kabla ya kutekeleza unyama huo.
Kulingana na Mkuu wa polisi mjini Mombasa Johnson Ipara uchunguzi umeanzishwa na imebainika kuwa Ann Waireri amekuwa akipitia mateso katika ndoa yake kwa muda mrefu.