Mkurugenzi mkuu wa Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la MUHURI Hassan Abdille amesema ufisadi katika Serikali za Kaunti humu nchinibado ni kikwazo kikuu katika mchakato wa maendeleo mashinani.
Abdille amesema serikali za Kaunti zimeshiriki ufisadi katika idara zote zikiwemo kuajiri watu, ununuzi wa bidhaa, utoaji wa huduma msingi miongoni mwa idara nyinginezo muhimu.
Abdille amesema ni lazima Kaunti za hapa Pwani zijitenge na ufisadi na upendeleo katika utoaji wa zabuni hasa kwa Vijana na akina mama.
Abdille amezitaja harakati zinazofanywa na Rais Uhuru Kenyatta, Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Noordin Hajj, Mkurugenzi mkuu wa Idara ya upelelezi George Kinoti kama mwafaka, akisema ni sharti Magavana waunge mkono juhudi hizo.
Mtetezi huyo wa haki za kibinadamu hata hivyo anasisitiza adhabu kali kwa washiriki wote wa ubadhirifu wa mali ya umma.