Shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURI limeitaka serikali kuhakiksaha inajitolea kikamilifu katika vita dhidi ya ufisadi ili kuhakikisha raslimali za taifa hili zinamfaidi mwananchi.
Kwa mujibu wa Afisa wa kitengo cha dharura katika Shirika hilo Francis Auma kashfa za mara kwa mara za ufisadi zinazoshughuduwa nchini zinadhirisha wazi kuwa serikali bado haijaweka msukumo wa kutosha katika kupiga vita ufisadi.
Akizungumza kwenye mkao wa kuhamasisha umma kule Bombolulu kaunti ya Mombasa, Auma ameitaka serikali kuu na zile za kaunti nchini kuwaachisha kazi wafanyikazi wanaojihusisha na ufisadi.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.