Shirika la utetezi wa haki za kibnadamu nchini la MUHURI limewataka viongozi wa kidini kujitokeza na kusaidia idara za serikali katika kupiga vita ufisadi nchini.
Kulingana na afisa wa kitengo cha dharura katika shirika hilo Francis Auma mabilioni wa fedha yameporwa na viongozi wa kidini humu nchini wamesalia kimya licha ya kuwa na ushawishi mkubwa katika taifa hili.
Afisa huyo wa shirika la MUHURI aidha amesema kuwa endapo viongozi wa kidini na wananchi watashirikiana katika kupiga vita ufisadi jinamizi hilo litakomeshwa.
Kauli yake inajiri huku sakata za ufisadi zikiendelea kushughudiwa nchini.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.