Taarifa na Sammy Kamande
Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la MUHURI linataka majaji watatu wa mahakama ya Rufaa Erastus Githinji, Martha Koome na Fatuma Sichale kuchunguzwa kufuatia uamuzi wao wa kupinga kesi iliyowasishwa na shirika hilo kuhusu uteuzi wa makarani 290 waliyosimia marudio ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2017.
Mwenyekiti wa shirika hilo Khelef Khalifa amesema kwamba majaji hao watatu hawakuzingatia sheria yoyote na walifanya hivyo baada ya kuongozwa na aliyekuwa rais wa mahakama hiyo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa sheria nchini Paul Kihara.
Kulingana na Khalifa, misingi ya katiba ilipuuzwa kwani Majaji hao hawakuwa pamoja wala hawakuianisha uamuzi wowote ule bali walikabidhiwa uamuzi huo wa kupinga uamuzi wa Jaji wa mahakama kuu George Odunga aliyeweka wazi kwamba uteuzi wa Maafisa hao na Manaibu hao ulifanywa kinyume cha sheria.
Khalifa ametaka tume ya huduma ya mahakama nchini JSC kuwachunguza Majaji hao watatu anaodai wanatumiwa na Wanasiasa katika kutekeleza majukumu yao badala ya kuzingatia sheria na kuwatendea Wananchi haki.
Kwa sasa Shirika hilo limeapa kuwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kushinikiza kuchukuliwa hatua kwa Majaji wa mahakama ya rufaa Erastus Githinji, Martha Koome na Fatuma Sichale kufuatia uamuzi wao tata wa kuruhusu Maafisa 290 waliyoteuliwa na tume ya IEBC kusimamia marudio ya uchaguzi wa urais mwaka 2017.