Mkurugenzi mkuu wa Shirika la utetezi wa haki za binadamu nchini la MUHURI Hassan Abdille amesema kuwa ni sharti serikali kuu na zile za kaunti zishirikiane ili kuhakikisha maendeleo ya ugatuzi yanamfikia mwananchi mashinani.
Akizungumza Mjini Mombasa Abdille amesema kwamba iwapo Serikali hizo mbili zitatengana kisiasa mwananchi atazidi kuhangaikia katika kupata huduma muhimu.
Abdille amesema kwamba ni jambo la kusikitisha kuona wakenya na hususan wakaazi wa Pwani hawajihusishi na ugatuzi mashinani, huku viongozi wa Kaunti wakinufaika na mfumo huo.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.