Shirika la kutetea haki za Binadamu la MUHURI limeipa Idara ya Upeleleni nchini makataa ya siku 7 kuwaeleza wakenya chanzo cha kifo cha mwanafunzi wa Chuo kikuu cha cha Rongo kilichoko kaunti ya Migori Sharon Otieno, anayedaiwa kuuwawa kupitia hali ya kutatanisha.
Afisa wa kitengo cha dharura katika Shirika hilo Francis Auma, amesema Shirika hilo limeghadhabishwa na kifo cha Sharon ambaye alikuwa akisomea taaluma ya maswala ya afya katika chuo hicho.
Auma ameitaka Serikali kupitia kwa idara ya usalama kuhakikisha wahusika wa kifo cha mwanafunzi huyo wanakabiliwa kisheria.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi tawi la Mombasa wamelaani vikali hatua hiyo na kuishinikiza serikali kufanya uchunguzi wa kina na kuwakabili wanahusika.
Taarifa Cyrus Ngonyo.