
Shirika la kutetea haki za kibinadamu Muhuri limezitahadhahari shule zote humu nchini kujitenga na dhana ya kwamba wanafunzi wa dini ya kislam kutovaa vazi la hijab wanapokuwa shuleni.
Akiongea mjini Mombasa mwenyekiti wa shirika hilo Khelef khalifa amesema kuwa hatua hiyo ya baadhi ya shule kutenga wanafunzi kupitia maswla ya dini huenda ikaleta chuki baana ya waumini wa dini ya kislamu na kristo.
Aidha amesema kuwa nijukumu la shule za humu nchini kujitenga na kasumba za kugawanya wanafunzi kidini kwani huenda ikaipa nafasi kundi la kigaidi la Al-shabab kuendeleza visa vya uhalifu humu nchini sawia na kuathiri viwango vya elimu.
Haya yanajiri baada ya mahakama ya upeo nchini kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na shule ya upili ya St Paul kiwanjani kutaka wanafunzi wazivae vazi la hijab baada ya kubainika kwamba kesi hiyo haikufuata sheria hitajika.
Taarifa na Hussein Mdune.