Afisa wa maswala ya jinsia na haki za watoto katika Shirika la MUHURI, Topista Juma amesema wanawake hapa Pwani wanapaswa kuhamasishwa kuhusu athari za ugaidi na itikadi kali.
Topista anasema wanawake wamejipata katika mtego huo kutokana na ukosefu wa ufahamu, akiitaja hali hiyo kama hatari kwa maisha ya wanawake hapa Pwani.
Akizungumza mjini Mombasa, Topista amesema iwapo hamasa na elimu ya kutosha itatolewa kwa wanawake kuhusu athari za ugaidi na itikadi kali, basi Wanawake hapa Pwani watakwepa mtego huo na kuzikinga jamii zao.
Kulingana na Topista, hamasa hizo vile vile zinapaswa kulenga zaidi shule na walimu kwani vijana wamejipata katika maswala ya itikadi kali kupitia kwa hadaa za washirika wa mitandao hiyo.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.