Shirika la kutetea haki za kibnadam la MUHURI linataka maafisa wa usalama wanaohusika na mauaji ya watu wasiokua na hatia pwani kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Afisa wa maswala ya dharura, haki na sheria katika shirika hilo Fahad Changi anawataka maafisa husika kukamatwa.
Changi amesema haya katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya ukanda wa pwani wakati wa kutoa miili ya mwanafunzi Samuel Odemba Odhiambo na ule wa Caleb Espino Otieno anayedaiwa kuuwawa mikononi mwa maafisa wa polisi wa Changamwe.
Taarifa Gabriel Mwaganjoni.