Story by: Gabriel Mwaganjoni
Dini nyingi nchini zimekosa kushirikisha sauti za akina mama na vijana hali inayowafanya watu hao kukandamizwa katika jamii na maswala ya dini vile vile.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la KECOSCE Phyllis Muema amesema kubaguliwa kwa mwanamke na kijana katika maswala ya dini, majadiliano kuhusu mafunzo na mwelekeo wa kidini ni kati ya mswala yaliowasukuma vijana katika uhalifu, itikadi kali na ugaidi.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Phyllis amesema kuna baadhi ya maswala kama vile ukeketaji ambao umewaumiza wasichana wadogo na akina mama hasa katika kaunti za Tana river na Taita Taveta japo viongozi wa kidini wamelinyamazia swala hilo.
Wakati uo huo, amehimiza uiano wa kidini, akiwataka viongozi wa dini mbalimbali nchini kuleta uiano wa kidini hali itakayodhibiti malumbano, ubaguzi na chuki za kidini katika jamii.