Story by Gabriel Mwaganjoni-
Viongozi wa mrengo wa Kenya Kwanza wamedai kwamba kuhangaishwa kwa maafisa wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC ni njama ya wapinzani wao wa kisiasa kushinikiza kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Viongozi hao wakiongozwa na Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi wamesema uchaguzi mkuu wa Agosti, 9 hauwezi kubadilishwa kwa sababu ya njama ya watu wachache nchini.
Mudavadi amesema ni makosa kisheria kwa mtu yeyote yule kuwahangaisha maafisa wa Tume ya IEBC kwani Tume hiyo ilibuniwa kikatiba kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi huru na haki na kwa manufaa ya wananchi.
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Kinara mwenza wa mrengo wa Kenya Kwanza amesisitiza haja ya tume ya IEBC kuwa huru ili kutekeleza majukumu yake kikamilifu.