Story by Gabriel Mwaganjoni –
Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi amewataka wanawake humu nchini kusimama kidete na kupigania nafasi yao katika maswala mbalimbali yanayofungamana na uongozi.
Mudavadi amesema wanawake wana uwezo mkubwa wakuongoza katika nyanja mbalimbali na akawahimiza wasilegeze kamba katika azma yao ya kuhakikisha wanasimamia idara mbalimbali Serikali.
Mudavadi amesema jina la Jaji mkuu aliyependekezwa Martha Koome lipo mbele ya bunge la kitaifa tayari hiyo na hatua ni muhimu kwa wanawake kunyakua wadhfa wa Jaji mkuu wa taifa hili.
Hata hivyo, Kiongozi huyo anahimiza ushirikiano wa hali ya juu kati ya wanawake na wanaume na kuwataka wote kuweka maslahi ya mwananchi mbele katika kuimarisha maisha ya mkenya mashinani.