Kinara wa chama cha Amani National Congress (ANC) Msalia Mdavadi amewahimiza wakenya kudumisha amani msimu huu wa sherehe za mwisho wa Mwaka.
Akizungumza mjini mombasa mdavadi amehoji kuwa msimu huu ni wa kusaidia familia zisizojiweza sawia na wananchi hivyo basi akawasihi wakenya kujitenga na visa vya vurugu.
Hata hivyo Amewataka madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani hususani msimu huu wa sherehe kwani amesema wakenya wengi wanaelekea makwao kujiunga na familia zao kwa minajili ya sherehe za mwisho wa mwaka.
kwa upande wake askofu mkuu wa kanisa katholiki jimbo la mombasa Martin Kivuva amehimiza umoja kwa viongozi wa humu nchini ilikuona kwamba taifa la Kenya linakuwa na amani msimu huu wa sherehe za mwisho wa Mwaka.
Taarifa na Hussein Mdune.