Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi ameweka wazi kwamba mfumo wa siasa ulikamilika na viongozi wanapaswa kuwajibikia majukumu yao mashinani.
Mudavadi amesema mabishano ya kisiasa hayatasaidia katika kudhibiti makali ya ukame yanayolikumba taifa hili kwa sasa na badala yake viongozi wa mirengo yote ya kisiasa wanafaa kushirikiana katika kuwasaidia wakenya.
Kiongozi huyo amehoji kwamba Serikali ya Kenya Kwanza haitambagua mtu yeyote wala kumshurutisha kujiunga mrengo wowote wa kisiasa na badala yake kuwashirikisha wakenya katika kuyatekeleza majukumu yao kwa taifa.
Wakati uo huo ameapa kushirikiana na viongozi wa mirengo yote nchini katika kuhakikisha huduma msingi za Serikali zinamfikia mwananchi mashinani, huku akiwataka wakenya kuwaripoti maafisa wazembe kwa idara husika ili wachukuliwe hatua.