Story by Gabriel Mwaganjoni –
Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi ametaka kuangaliwa upya kwa sheria za soko la Mashariki na katika upembe mwa Afrika- COMESA ili kuhakikisha sheria za kuingiza sukari nchini zinafuata.
Mudavadi amesema kutozingatiwa kwa sheria hizo kumepelekea viwanda vya humu nchini kufifia kufuatia kuingizwa kwa sukari kiholela katika soko la humu nchini.
Mudavadi amesema ni sharti Serikali iweke mikakati inayostahili katika kulinda raslimali ya sukari nchini akisema hali inavikumba viwanda vya sukari hasa katika maeneo ya Magharibi mwa Kenya ni ya kusikitisha.
Kwa sasa, Mudavadi anataka hazina maalum iliyokuwa imebuniwa na Serikali ili kusimamia sekta ya sukari kuzinduliwa upya na kuidhibiti sekta ya sukari nchini.