Story by Gabriel Mwaganjoni –
Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi ameitaka serikali kupitia Wizara ya Kawi nchini kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa sekta ya Kawi na kuibuka na suluhu la kupunguza bei ya mafuta.
Mudavadi amesema wakenya wanapitia hali ngumu ya maisha kutokana na athari za janga la Corona, akisisitiza haja ya serikali kulishuhulikia swala hilo ili wakenya waweze kukidhi hali yao ya maisha.
Akizungumza wakati alipowatembelea waathiriwa wa moto katika eneo la Gatina, Stage Two, na Kawangware jijini Nairobi, Mudavadi amesema iwapo swala hilo halitashughulikiwa basi uchumi wa nchi utazidi kuwa mgumu kwani bidhaa nyingi nchini zitapanda bei.
Mudavadi hata hivyo amewarai wakenya kuunga mkono azma yake ya kuwania kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu ujao, akisema ili taifa hili liimarike kichumi linahitaji viongozi waadilifu na wawajibikaji.