Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mrengo wa Kenya Kwanza umeendeleza kampeni zake za kuingia ikulu mnamo Agosti, 9, huku Kinara wa Chama ca ANC Musalia Mudavadi akimshmbulia Rais Uhuru Kenyatta akidai Uhuru amepoteza mwelekeo kama kiongozi wa nchi.
Katika misururu ya mikutano ya kisiasa kaunti ya Narok, Mudavadi aliyeandamana na Naibu rais William Ruto, Kinara wa Chama cha Kazi Moses Kuria, yule wa Ford-Kenya Moses Wetangula miongoni mwa viongozi wengine, Mudavadi amesisitiza kwamba Rais Kenyatta hatowalazimisha Wakenya kumchagua Odinga.
Mudavadi amewataka Wakenya kuwa makini pindi uchaguzi mkuu wa Agosti 9 unavyozidi kuwadia.
Kwa upande wake, Kinara wa Ford Kenya Moses Wetangula amehoji kwamba kila mkenya ana fursa ya kubadilisha uongozi uliyopo kwa sasa akiwasihi Wakenya kutekeleza mabadiliko ya kiuongozi nchini pindi ifikapo Agosti 9 wakati wa uchaguzi mkuu.