Story by Gabriel Mwaganjoni-
Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi amesema wakenya wamejikwamua kimawazo na kimtazamo na hawawezi kulaghaiwa tena na wanasiasa.
Kinara huyo wa mrengo wa kisiasa wa Kenya Kwanza ameonekana kumlenga Rais Uhuru Kenyatta huku akisema Rais Kenyatta hana mamlaka yoyote ya kuwalazimisha wakenya wamchague Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kama Rais wa taifa hili.
Mudavadi amekariri kwamba taifa hili linagubikwa na ufisadi, akihoji kwamba ni kupitia Serikali ya Kenya Kwanza ndio itaukabili ufisadi.
Akigusia swala la usajili wa laini za simu, Mudavadi amesema kuna njama fiche ambayo mamlaka ya mawasiliano nchini CA inastahili kuweka wazi kuhusu zoezi hilo.