Picha kwa Hisani
Kinara wa chama cha ANC Musali Mudavadi amewataka maseneta wote kujitenga na malumbano ya kisiasa na badala yake kupigania maslahi ya wananchi kwa kuhakikisha kuna usawa katika ugavi wa fedha kwa serikali za kaunti.
Akizungumza hapo jana Mudavadi amesema mfumo wa ugavi wa mapato katika kaunti umewekwa wazi kwenye Katiba ya nchi na ni vyema iwapo vipengele vyote vinavyofungamana na ugavi wa mapato vitazingatiwa.
Mudavadi amesema mabishano yanayoendelezwa katika bunge la Seneti kuhusu ugavi wa mapato yanaathiri mchakato wa maendeleo nchini kwani usambazaji wa fedha kutoka serikali kuu hadi zile za kaunti unacheleweshwa.
Kiongozi huyo hata hivyo ametaka maafikiano ya haraka kufanyika katika bunge la Seneti ili kuhakikisha fedha za maendeleo zinasambazwa kwa serikali za kaunti.