Picha kwa Hisani –
Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi ameitaka Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kuwajibikia majukumu yake ili kuiwezesha Serikali kuwakabili wafisadi nchini.
Mudavadi amesema ni wazi kuwa tume hiyo imezembea katika kutekeleza majukumu yake hali ambayo inawapa nguvu wafisadi kuendelea kupora mali ya umma.
Akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa katika maeneo ya magharibi mwa Kenya, Mudavadi amesema ni lazima tume hiyo itekeleza uchunguzi wa kina na kuwanasa wafisadi.
Akigusia sakata ya ufisadi ya KEMSA, Mudavadi ameukosa uchunguzi unaoendelezwa katika KEMSA kama aibu kwa tume hiyo, akiitaka tume hiyo kujizatiti katika kulinda mali ya wakenya.